WATANZANIA TUSIPOTOSHWE KUHUSU THE ROYAL TOUR, WASOMI WA FILAMU NA WAIGIZAJI MSIKAE KIMYA, ELEZENI KUHUSU 'PRIMARY RIGHT' NA 'SECONDARY RIGHT' KWENYE UIGIZAJI

NA EMANUEL MARTINE (0623712600)

MOSI kuna watu wanahoji kuhusu umiliki wa The Royal Tour. Niwafahamishe kuwa, madhumuni ya The Royal Tour ni kuitangaza nchi na vivutio vyake na kuionesha Dunia kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania.
Kampuni ya Peter Greenberg sio wamiliki wa kila kitu. Umiliki kwenye uigizaji kuna hati miliki na hati shiriki (kwenye uigizaji kuna primary right na secondary right).

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.SAMIA SULUHU HASSAN ametimiza malengo ya kuitangaza nchi yetu, kuvutia watalii kwenye vivutio vyetu na kuisemea mema nchi yetu ili kupata wawekezaji kwenye sekta mbalimbali nchini.

Peter Greenberg kwenye The Royal Tour wamepewa kazi ya kumiliki katika hati miliki kwa sababu ndio wenye jina la THE ROYAL TOUR na Tanzania ni nchi ya tisa kutumia jina hilo, ingekuwa jina sio The Royal Tour wasingepewa hati miliki ya The Royal Tour na pia wamepewa kusambaza kwenye TV 360 za Marekani na Dunia ijue kuwa kuna nchi inaitwa Tanzania.

Rais SAMIA SULUHU HASSAN na Serikali wana hati miliki ya ushiriki na kusambaza pamoja na haki zote za kufanyia chochote filamu hiyo ya The Royal Tour.

Kwa nini hati miliki kwenye The Royal Tour wamepewa kampuni ya Peter Greenberg, ni kwa sababu wao ndio waanzilishi wa jina la THE ROYAL TOUR kwa nchi zaidi ya tisa.

Pili, kwanini kampuni ya Amazon imepewa kuuza??

Kwa sababu ndio wauzaji wakubwa wa filamu mbalimbali kutoka kokote, tunanunua CD au movie mbalimbali kutoka Amazon na hata Wewe unayesoma ujumbe huu kama sio wewe familia yako kila siku wanaenda kurusha movie pale Amazon.

Lengo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitangaza nchi, kupitia Amazon wadau wengi wanaweza kufika kununua CD hapo.

Baada ya uzinduzi utakaofanywa Dar es Salaam leo tuna amani TV mbalimbali za Tanzania zitakuwa zinaonesha bure filamu hiyo.

Naomba watanzania tusiposhwe hii The Royal Tour ni kazi ya sanaa kama zilivyo kazi za sanaa zingine,MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN amecheza filamu hiyo, alivua URAIS wake ili aweze kufanya kazi ya sanaa kwa weledi.

Muigiza ndani ya The Royal Tour ana haki shiriki zote na ana haki kufanyia chochote filamu hiyo na kokote pale.

The Royal Tour inaweza kuwa inaoneshwa hata kwenye mabanda ya sinema kama movies zingine zinavyoneshwa.

KATIKA HILI LA THE ROYAL TOUR, TUSHIKAMANE KAMA WATANZANIA

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news