NA MWANDISHI WETU
WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umehamasisha wananchi kutembelea banda lake katika Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayoendelea katika Uwanja wa Mwahako jijini Tanga ili kupata huduma mbalimbali.
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Mheshimiwa Dkt.Ashatu Kijaji akipata maelezo juu ya huduma zinazotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kutoka kwa Afisa Leseni, Bi.Saada Kilabula. Ni katika Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii ambayo yameanza Mei 28, 2022 jijini Tanga. Maonesho hayo yameanza tarehe 28 Mei, 2022 katika Uwanja wa Mwahako jijini Tanga na yanatarajiwa kufikia tamati Juni 6, 2022.(Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano-BRELA).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara,Dkt.Hashil Abdallah akipata maelezo ya namna Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inavyotoa huduma zake kwenye maonesho ya tisa ya biashara na utalii yanayoendelea mkoani Tanga kuanzia tarehe Mei 28, 2022.
Msajili Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Selemani Selemani akitoa usaidizi kwa Bi. Hafsa Kwallow juu ya namna ya kujaza Katiba ya kampuni kwenye Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwenye Maonesho ya Tisa ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga hadi tarehe 6 Juni, 2022. Katika maonesho hayo BRELA inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara Kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa ORS.
Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Julieth Kiwelu akitoa elimu ya Hataza kwa Bw. Musini Abdallah katika Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga. Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda Leseni ya Biashara kundi A, na mafunzo pamoja na usaidizi juu ya matumizi ya mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS).
Afisa Tehama Msaidizi kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Hillary Mwenda akitoa usaidizi wa usajili wa Jina la Biashara kupitia mfumo wa usajili kwa njia ya Mtandao (ORS) kwa Bw. Emmanuel Mallya kutoka Korogwe-Tanga kwenye Maonesho ya Tisa (9) ya Biashara na Utalii yanayofanyika katika Uwanja wa Mwahako mkoani Tanga.
Katika maonesho hayo BRELA pia inatoa huduma za Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, kupata Leseni ya Kiwanda, Leseni ya Biashara kundi A, kupata Hataza na kutoa mafunzo pamoja na usaidizi juu ya kutumia mfumo wa ORS.