Waziri Mkuu: Wanahabari zingatieni miiko na kanuni za uandishi

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameoa wito kwa wanahabari kuzingatia miiko na kanuni za kimaadili zinzoongoza taaluma hiyo na kuweka kipaumbele kwenye ustawi wa Taifa badala ya maslahi binafsi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (Ejat), katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, Mei 28, 2022.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Amesema kuwa wanahabari wanapaswa kutambua kuwa habari ni bidhaa ya jamii na siyo bidhaa ya kuuzwa hivyo wanawajibika kwa umma na wanapaswa kutetea maslahi ya Taifa. “Wanahabari wenye weledi na wanaozingatia maslahi ya Taifa ni chachu ya kutimiza dhima ya kuleta mchango kwa taifa.”

Amesema hayo leo Mei 28, 2022 wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Hafla ya Utoaji Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) katika Hotel ya Serena Dar es Salaam.

“Haiba na taswira yenu nzuri huwa inaharibiwa na uandishi wa habari usiofuata maadili ya uandishi wa habari, kuandika habari ambazo hazijafanyiwa utafiti, kuandika habari za uongo na za kupotosha zenye lengo la kuichafua Serikali au mtu mmoja mmoja”
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Mwanahabari Nguli, Ndimara Tegambwage hundi ya Shilingi Milioni kumi baada ya kutambuliwa na kupewa tuzo ya Maisha ya Mafanikio katika Uandishi wa Habari (Laja) 2022. alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (Ejat), katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, Mei 28, 2022. kushoto ni Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania Kajubi Mkajanga (katikati) (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ameongeza kuwa vitendo hivyo ni kinyume na kanuni za maadili ya taaluma yenu zinazowataka kutafuta ukweli wa habari kabla ya kuzitangaza na kuepuka kutoa taarifa za uongo zilizopikwa kwa lengo la kudanganya umma, kupotosha ukweli au zenye nia ya uchochezi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye, wakati alipomwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan katika hafla ya utoaji tuzo za umahiri wa uandishi wa habari Tanzania (Ejat), katika Hotel ya Serena Jijini Dar es Salaam, Mei 28, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Awali akimkaribisha Mheshimiwa Waziri Mkuu, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Nape Nnauye ametoa wito kwa waandishi wa Habari wa Tanzania kushiriki kwa kuwasilisha kazi zao za habari katika kuwania tuzo za kimataifa kutokana na kazi nzuri wanazofanya ndani ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news