NA OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewasisitiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia kikamilifu utekelezaji wa mikakati yote ya sekta ya kilimo inayotekelezwa kwenye halmashauli ili kuleta mageuzi katika sekta ya kilimo na kuongeza tija kwa wakulima.

Bashungwa amesema, Ofisi ya Rais-TAMISEMI itaendelea kuimarisha ushirikiano na Wizara ya Kilimo ili kuhakiksha dhamira ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ya kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo yanatimia kupitia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Aidha, Bashungwa amepongeza mfumo wa sasa wa mauzo ya kahawa kufanyika kwa njia ya mnada ngazi ya vyama vya msingi ambao utamkomboa mkulima wa zao hilo na kuondokana na mfumo wa awali uliokuwa unawanufaisha watu wachache na sio wakulima.