NA DIRAMAKINI
MKUU wa Wilaya ya Ubungo, Heri James amewataka viongozi wa dini nchini kutumia nafasi zao kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa, kwani kufanya hivyo kunatoa fursa kwa Serikali kuwafikia wananchi wake kimaendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James (kulia) akikabidhi makusanyo kwa Mwenyekiti wa Chama kipya cha Umoja wa Wababa Kanisa la Anglicana Achidikonari ya Ubungo (UBAKI) Moses Manyatta (kushoto) yaliyokusanywa kutoka kwa washarika na waumini wa kanisa hilo (hawamo pichani) wakati wa sherehe za kuzindua rasmi Umoja huo zilizofanyika leo Juni 11,2022 katika kanisa la Mtakatifu Batolomayo Ubungo Jijini Dar es Salaam.
Amesema, mwaka huu Agosti 23 ni mwaka wa sensa hivyo ni vema viongozi wakahamasisha wananchi wao na kuwakumbusha umuhimu wa kuhesabiwa ukizingatia zoezi hilo linafanyika kila baada ya miaka kumi.
Mkuu wa Wilaya ya Ubongo Kheri James akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake katika hafla hiyo muda mfupi baada ya kuzindua rasimi Umoja wa Chama cha Wababa (UBAKI) wa Kanisa Anglicana katika Wilaya ya Ubungo.
DC James ametoa kauli hiyo leo Juni 11, 2022 mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa umoja wa Chama cha Wababa (UBAK) wa Kanisa la Angalikana Archidikonary ya Ubungo uliofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Barthromayo wilayani humo.
Wanachama wa UBAKI na wageni mbalimbali waalikwa wakiwa kwenye maandamano maalum yaliyoanza mapema Asubuhi ya leo Juni 11,2022 kutokea Shekilango hadi kwenye kanisa hilo kwaajili ya Ibada fupi iliyofanyika Kanisani hapo kabla ya kuanza shamrashamra za uzinduzi rasmi wa Umoja huo.
"Serikali hususani Wilaya yangu ya Ubungo tuna mashirikiano mazuri na Kanisa la Anglikana kupitia viongozi wake, ni matumaini yangu hata katika hili la UBAKI tutaendelea kushirikiana pasipo shaka.
"Ndungu zangu kupitia Umoja huu tuimarishe malezi kwa vijana ,maadili ,na tuendelee kukemea wizi,ufisadi,dhuluma,ukatili na uhujumu kwani haya yote ni roho zisizokubarika katika jamii yetu"amesisitiza James.
Mwnyekiti wa UBAKI Mosses Manyatta akizungumza akelezea majukumu ya chama hicho mapema mara baada ya kuwasili mgeni rasmi kwenye hafla hiyo iliyofanyika leo Juni 11,2022 jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Kasisi Kiongozi wa Kanisa la Angalikana Dayosisi ya Dar es Salaam, Richard Kamenya pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha UBAKI, Moses Manyatta wamesema pamoja na mambo mengine yote lakinin pia watatumia umoja huo kuhamsisha waumini kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa linalotarajia kufanyika kitaifa Agosti 23 mwaka huu.
Viongozi wa UBAKI wakitambulishwa rasmi na kuwekwa wakfu kukiongoza chama hicho katika hafla hiyo. Pia wameipongeza na kuishukuru Serikali kwa ushirikiano mkubwa wanaoendelea kuutoa kwenye Taasisi za dini hivyo wao kama viongozi jukumu lao kubwa ni kuendelea kusimamia utulivu uliopo.
Katika uzinduzi huo wa Chama cha Umoja wa Baba (UBAKI), Mkuu wa Wilaya hiyo ya Ubungo, Heri James amechangia shilingi laki tano (500,000) kwa ajili ya kutunisha ufuko wa umoja huo.