NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji ni Serikali kamili katika maeneo yao. Sifa mojawapo ya Serikali yoyote ni kwamba inakuwa na uwezo wa kupata na kutumia fedha.
Serikali hupata fedha kwa kuwatoza raia wake kodi, ushuru na ada mbalimbali. Hali kadhalika, Halmashauri za Miji na Wilaya zina madaraka ya kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kwa jinsi sheria za nchi zinavyoruhusu.
Moja wapo ya manufaa ya kila mmoja kulipa mapato ya halmashauri kwa wakati ni pamoja na kusaidia uboreshaji na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo,jifunze jambo hapa;