Edwin Soko:Tuandike habari zinazohusu uendelevu wa fukwe,maziwa na bahari jamii iweze kutambua umuhimu wa kutunza mazingira ya majini na nchi kavu

NA SHEILA KATIKULA

WAANDISHI wa habari wametakiwa kuandika habari za takwimu zinazohusu uendelevu wa fukwe,maziwa na bahari ili jamii iweze kutambua umuhimu wa kutunza mazingira ya majini na nchi kavu.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maadhimisho ya Siku ya Uwazi wa takwimu yaliyoandaliwa na Ojadact kwa kushirikiana na Shirika la Open Knowledge Foundation.

Soko amesema, waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya kuisaidia jamii kutambua umuhimu wa katunza mazingira ya majini na nchi kavu kwa manufaa ya uchumi wa nchi.

Amesema, takribani asilimia 57 ya uchumi wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, unategemea shughuli za maziwa na bahari hivyo jamii kutowajibika kwenye utunzaji wa mazingira inaweza kusababisha joto kali duniani na kupelekea fukwe kupotea.
Naye Mratibu OJADACT, Lucyphine Kilanga amesema ili jamii iweze kutambua umuhimu wa kulinda na kutunza mazingira ni vema waandishi wa habari kuandika habari za takwimu zinazotolewa na mamlaka mbalimbali zinazohusu ustahimilifu au uhimilivu wa fukwe za bahari na maziwa.

Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo,Leah Marco na Fredick Chibuga wameziomba taasisi za umma na mashirika binafsi mbalimbali yanayojihusisha na uhifadhi wa mazingira kuwajengea uwezo ili kuwasaidia kufuatilia masuala ya uhifadhi wa rasilimali zilizopo nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news