NA DIRAMAKINI
MAHAKAMA Kuu Dar es Salaam imetupa maombi ya Halima Mdee na wenzake kutokana na kasoro katika jina la mjibu maombi wa kwanza.
Halima ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) na wenzake waliomba kibali cha kupinga kufukuzwa uanachama wa Chadema katika mahakama hiyo.
Wajibu maombi walikuwa Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).
Chadema kupitia jopo la mawakili wake linaloongozwa na Peter Kibatala waliweka pingamizi wakiiomba Mahakama hiyo isiyasikilize maombi hayo, wakidai kuwa yana kasoro za kisheria huku wakibainisha hoja sita.
Nje ya Mahakama hiyo, Wakili wa Chadema, Peter Kibatala amefafanua kuwa Mahakama pia imetupilia mbali maombi ya msingi ya kutaka kupewa kibali cha kufungua kesi ya kupinga kuvuliwa uanachama.
Kibatala ameeleza kuwa miongoni mwa sababu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kukosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya Chadema iliyosajiliwa.
Kibatala ameeleza kuwa miongoni mwa sababu ya kutupiliwa mbali kwa maombi hayo ni kukosewa kwa jina la mjibu maombi namba moja ambaye ni Bodi ya Wadhamini ya Chadema iliyosajiliwa.