NA ASILA TWAHA, OR-TAMISEMI
SERIKALI imetoa kiasi cha shilingi billioni 4.1 kwa halamashauri nne zilizokidhi vigezo kuendeleza programu ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi nchini.

Hafla ya utiaji wa saini wa mikataba ya fedha umefanyika Juni 10, 2022 jijini Dodoma ambapo halmashauri zilizokidhi vigezo hivyo ni Manispaa ya Kigamboni, Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Manispaa ya Lindi na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Amesema, halmashauri nyingi bado kuna changamoto ya ardhi kwa kutokupangwa na hii hupelekea kutokea kwa migogoro kati ya wananchi na halmashauri kitu kinachosababisha kuzorotesha ukusanyaji wa mapato ya Serikali.

Pia amezielekeza halmashauri hizo kutumia fedha hizo kama zilivyoelekezwa isitokee fedha hizi kuenda kubadilishwa matumizi.
"Ofisi ya Rais-TAMISEMI kwa kushirikiana na wenzetu Wizara ya Ardhi tutazifuatilia, lengo la Serikali mzitumie na kuzirejesha kwa ajili ya halmashauri nyingine ziweze kufaidika,"amesisitiza.

Akiendelea kufafanua amesema, zipo baadhi ya halmashauri zilizopatiwa mkopo wamepima viwanja lakini mpaka sasa hawajaidhinisha kuuza kwa viwanja, pia amesema zipo Halmashauri wamepatiwa fedha hizo lakini mpaka sasa hawajaanza kuzitumia.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa (USEMI), Bw. Abdallah Chaurembo ameishukuru Serikali kwa kuridhia na kuendelea kutoa mikopo ya fedha kwa Halmashauri na amezitaka Halmashauri kutumia fedha hizo kwa malengo ili kuondoa hoja zinazotokea pindi kamati zinapoeenda kukagua na kujiridhisha kwa matumizi ya fedha walizopokea.