NA DIRAMAKINI
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI Prof.Riziki Shemdoe ameridhia kufanyika kwa uhamisho watumishi 1,048 wa kubadilisha vituo vya kazi pekee. Watumishi hao ni wale walioomba uhamisho kuanzia Mwezi Februari-Mei,2022.
Amewataka watumishi waliopata uhamisho huu kusubiria barua kwenye Halmashauri zao na sio kufika Ofisi ya Rais-TAMISEMI kufuata barua hizo.