NA SHEILA KATIKULA
VIONGOZI wa Kamati ya Amani mkoani Mwanza wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kupewa tuzo ya Babacar Ndiaye ya mwaka 2022 inayotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Hayo yamesemwa na Sheikhe Hassan Kabeke kwenye kikao cha viongozi ya Kamati ya Amani Mkoa Mwanza kinachowashirikisha viongozi wa dini mbalimbali.
Amesema, lengo la kikao hicho ni kumpongeza Rais Samia kwa kupewa tuzo na kutelekeza miradi mbalimbali inayoendelea sehem mbalimbali.
"Tunampongeza Rais Samia kwa kutoa Sh bilioni 100 kwa ajili ya kupunguza makali ya mafuta pamoja na kutoa Sh milioni10 kwa kila Mkoa kwa ajili ya kuwasaidia wamachinga.
"Kwenye miradi ya kimkakati ya Mkoa wa Rais Samia Suluhu ametoa Sh bilioni 339,655,579,831 fedha ambazo zimeenda kwenye ujenzi wa stendi ya mabasi na malori Nyamhongoro ambayo umefikia asilimia 100,ujenzi wa stendi ya Nyegezi umefikia asilimia 77,ujenzi wa soko la kisasa (soko kuu)umefikia asilimia 66.
"Fedha hizo zimeenda kwenye ujenzi wa jengo la abili kwenye uwanja wa ndege kwani umefikia asilimia 88,ujenzi wa Mv Mwanza umefikia asilimia 59,ujenzi wa daraja la kigongo busisi umefikia asilimia 42,"amesema Sheikh Kabeke.
Naye Askofu Charles Sekelwa amesema Rais Samia amepanua wigo katika kulijenga taifa na kuleta mahusiano ya kidipromasia baina ya nchi na nchi na kulitafanya taifa kutambulika duniani kote kupitia filamu ya Royal tour.
"Sisi Kama kamati ya maadili Mkoa wa Mwanza tumejiridhisha, tumechunguza, tumejipatia taarifa sahihi na tunayoyasema ndivyo yalivyo,"amesema Askofu Sekelwa.
Akitoa pongezi Askofu Sekelwa amesema Serikali ya Tanzania imetoa Sh bilioni 264 kwa ajili ya kuwalipa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi.
Naye mshauri kamati ya amani Mkoa Mchungaji Dk Jacob Mutashi amesema kuwa viongozi wa dini ni wabia na Serikali katika kukutana na kujadili amani ya nchi.
"Viongozi wa dini tuna watu katika nyumba za ibada tunaheshimika kwa sababu tunachokiagiza waumini wanafanywa niombee kila agizo lolote ambalo Rais Samia akitaka liwafikie watu kwa haraka na liwe na matokeo viongozi wa dini wahusishwe hata katika kupewa elimu",amesema Mchungaji Mutashi.
"Tunaendelea kuliombea taifa letu amani iliyopo indelee kuwepo pamoja na mshikamano baina ya madhehebu na dhehebu.
Mjumbe wa kamati hiyo Sikitu Abubakar amempongeza Rais Samia Suluhu katika anwani za Makazi kwani imeleta matokea chanya kwa taifa sanjari na kuandaa filamu ya Royal tour ambayo imeongeza watalii nchini.
Hata hivyo amewaomba watanzania wajitokeza kwa wingi kwenye zoezi la sensa linalotarajiwa kufanyika Agosti 23, mwaka huu