Usiwaze kufika viwanja vya Sabasaba ukitokea Mbagala jijini Dar es Salaam. Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka imekufikia!
Sensa ni nini?
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini na kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalum.
Aidha, kwa maana nyingine, sensa ni zoezi maalum lenye lengo la kupata idadi ya watu wote katika nchi, kwa umri na jinsia, mahali wanapoishi na hali yao ya elimu, hali ya ajira, hali ya vizazi na vifo na hali ya makazi.
Takwimu hizi za msingi ndiyo zinazoweza kuanisha mahitaji halisi ya wananchi yakiwemo makundi maalum yenye uhitaji maalum kwa mfano, watu wenye ulemavu, wanawake, watoto, vijana na wazee hivyo kurahisisha uandaaji wa sera na mipango ya maendeleo kulingana na uhitaji na mazingira yaliyopo.
Serikali inapofahamu idadi na makazi sahihi ya watu wake, inarahisisha kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuzifikia kaya au nyumba ambazo bado hazijapata nishati, kwa kuwa tayari Serikali inatambua zilipo na mahitaji yake.'Tanzania Sensa Agosti 23, 2022. Jiandae Kuhesabiwa'.