NA DIRAMAKINI
MISS Tanzania kwa mwaka 2022 Halima Kopwe ametoa rai kwa Watanzania wote kujitokeza kwa dhati kushiriki kuhesabiwa Agosti 23, mwaka huu ambapo zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litafanyika ambapo amesema sensa ina umuhimu mkubwa kwa uchumi na maendeleo ya nchi.
"Mimi kama Halima Kopwe nimejiandaa kuhesabiwa, nitaungana pamoja na Serikali na Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ili niweze kuhesabiwa mwezi wa nane mwaka huu. Nawahamasisha Watanzania wenzangu wote pia wajiandae kuhesabiwa itatusaidia sana kwenye uchumi wa nchi yetu...Mimi ni Halima Kopwe Miss Tanzania 2022 nimejiandaa kuhesabiwa,"amesema Halima Kopwe.