Mjadala maalum waonesha mwelekeo chanya kuelekea safari ya neema tupu Zanzibar

NA DIRAMAKINI

LEO Juni 25, 2022 Watch Tanzania kwa udhamini wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) na Airtel Tanzania imeratibu mjadala maalum uliongazia maendeleo ya miundombinu na faida za uwekezaji katika visiwa vinavyozunguka Zanzibar.

Kupitia mjadala huo, washiriki wametoa mawazo chanya ambayo yanatoa mwanga mpya katika kuiendea safari ya neema tupu Zanzibar, endelea;

Dkt. Khalid Mohammed

Unapoona mabati yamezungushwa au zile cranes za ujenzi hiyo ni maana kubwa kwamba nchi sasa inajengwa na hayo ndio maendeleo ndani ya Zanzibar.

Nchi yoyote ikiendeleza miundombinu kuna uhusiano moja kwa moja na kukuza uchumi, hiyo ni ishara kubwa ya maendeleo nchini.
Nahaat Mahfoudh

Bandari katika uchumi wa buluu ni kiungo muhimu katika kufikia malengo ya mkakati wa uchumi wa buluu
Bandari zote za Zanzibar zimejengwa katika kipindi cha mwaka 1920-25 hivyo ukilinganisha na mahitaji ya sasa kuna haja ya kuongeza ufanisi wa huduma za bandari.

Shariff Shariff

Kuna baadhi ya visiwa ambavyo tayari vilikua vimekodishwa, na kuna visiwa ambavyo vilikua havijakodishwa na kiukweli vingine vilikua havileti tija kwa nchi.
Hatutaki tutoe visiwa kwa wawekezaji ambao hawana tija, ndio maana tumependelea kuvitoa visiwa kwa wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kuviendeleza visiwa hivyo kwa tija. 

Tumetoa visiwa kumi (10) kwanza, na vigezo vya kupata tenda ya uwekezaji wa visiwa hivi imekua ni mtaji mkubwa wa muwekezaji, utunzaji mzuri wa mazingira na namna muwekezaji atashirikisha wananchi katika uwekezaji wake.

AYOUB MAHMOUD

Kisiwa cha Mnemba kimekodishwa kwa zaidi ya miaka 26 na sasa awamu ya 8 ndio motisha zaidi ya uwekezaji huo inazidi kuonekana.
Uwekezaji wa kisiwa cha Mnemba umewezesha upatikanaji wa kuendelezwa kielimu kwa vijana 63 ambao wamelipiwa huduma za elimu na kisiwa cha Mnemba.

TOGOLAN MAVURA

Uwekezaji wa visiwa vidogo Zanzibar sio jambo jipya, nchi kama Mauritius inapata watalii milioni 1 kwa mwaka na inachangiwa na uwekezaji wa visiwa .
Visiwa 10 bora Africa vinamilikiwa na taasisi/watu binafsi, na Rais Mwinyi amekuwa jasiri katika kuruhusu ukodishwaji wa visiwa hii kwa manufaa makubwa zaidi.

ANISA MBEGA

India ina visiwa vingi ambapo visiwa vidogo hukodishwa kwa wawekezaji ili kuendeleza miundombinu ya visiwa hivyo ambapo serikali ya visiwa hivyo inakua imeshindwa kuviendeleza kwa kukosa fedha na teknolojia.
Moja ya kigezo cha uwekezaji wa visiwa India ni pamoja na muwekezaji kutimiza majukumu ya utuzanji mazingira, kama ambavyo imekua katika vigezo vya kukodisha visiwa vya Zanzibar 

FATMA KHAMIS

Tuko kwenye tafiti kutazama uwezo wa Zanzibar kuhimili ongezeko la watalii zaidi kwa huduma mbalimbali bila kuathiri mazingira yetu.
Aina ya miradi ambayo imeruhusiwa kwenye visiwa hivi vinavyokodishwa ni ile ambayo italeta tija kwa jamii bila kuathiri mazingira yaani pande zote zinanufaika na uwekezaji huu.

GEN. GAUDENCE MILANZI

Elimu ni muhimu katika uwekezaji wa visiwa ili kuondoa dhana ya kutofahamu uzuri wa uwekezaji wa bahari kwa watu wetu.
Tafsiri sahihi zaidi ya Uchumi wa Buluu ni pamoja na matumizi bora ya rasilimali za bahari na Zanzibar inatekeleza hili kwa ufanisi kupitia uwekezaji huu wa visiwa.

JONATHAN

"Our design of accomodation is very well reflecting the Zanzibar environment and since it is the destination of Tourists we are dedicated to caring our communities and staffs.

Our investment model has considered partnering with the government and never to dictate what should be done, also offering education and other services to the surrounding community".

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news