NCCR-Mageuzi hakutabiriki

NA DIRAMAKINI
 
WAKATI Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini akimtaka mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia na kundi lake kujipanga kwa hoja kujibu mashtaka anayotuhumiwa kuyafanya, mwenyekiti huyo amemjibu hawezi kujiingiza kwenye vurugu hizo.

Akizungumza Juni 28, 2022 Mbatia amesema, Katiba ya chama hicho inamtambua yeye kama mtendaji wa shughuli zote na ni msemaji mkuu wa taasisi hiyo huku akiwasisitiza kufuata taratibu walizojiwekea.

“Utaratibu ukiwekwa mahali usipoufuata ni fujo kwa mujibu wa chama Msemaji mkuu na mtendaji mkuu ni mimi hayo yote wanasema wafuate utaratibu Jamaes Mbatia hayupo juu ya Katiba ya Chama wala juu ya sheria hizi ni fujo na nisingependa kuingia kwenye fujo zao,”amesema Mbatia.

Selasini katika mkutano wake na vyombo vya habari amesema, anashangaa kuona kundi linaloongozwa na Mbatia kutumia muda mwingi kutukana watu na kueleza hoja ambazo hazina ukweli badala ya kujipanga kujibu tuhuma zao kwenye mkutano mkuu.

“Tunachosema Mbatia na kundi lake waache kutunga propaganda za kitoto za udini, ukanda, ukabila na waache kugawa nchi hii kwa pande mbili za muungano wajipange kwa hoja wajibu kwenye mkutano mkuu,”amesema.

“Nafasi ipo wakae chini hawa wajumbe wanaowaita wajumbe, wataitwa kusikiliza hukumu yao badala ya kujikita kuwaita watu wahuni wajipange kujibu hoja kwa makosa saba wanayotuhumiwa, hiki ni chama cha watu si mali ya Mbatia,”amesema Selasini.

Selasini ambaye kwenye mkutano huo kwa mara ya kwanza amejitambulisha kama mwenyekiti wa bodi ya wadhamini wa chama hicho amesema, karibuni walifanya kikao cha dharura na baadaye waliafikiana kuiandikia barua Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenda kuchukua taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ofisi ya Msajili ili kuwahojiwa Mbatia na kundi lake.

Amesema, mkaguzi mkuu alifanya uchunguzi kwenye chama hicho kupitia kibali cha Msajili wa Vyama vya Siasa baada ya malalamiko ya wanachama na ulijikita kwenye hoja saba ambazo ziliwafanya wajumbe wa halmashauri kufanya kikao cha kumsimamisha Mbatia na wenzake kupisha uchunguzi.

“Katika barua hiyo amebainisha kuwa Mbatia na kundi lake wanatuhumiwa kujinufaisha na mali za chama chetu kinyume na taratibu na kutumia vibaya madaraka kwa muda wakipindi chote cha miaka 22 ya utawala wake ikiwemo kuwasimamisha makatibu wakuu saba na kuteua viongozi kinyume na sheria.

“Tunamsihi Msajili wa Vyama vya Siasa kuonesha ushirikiano kwa TAKUKURU kwa kuwa CAG alishamaliza kazi yake na kuikabidhi ripoti ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa kupitia mapendekezo yaliyotolewa tunaomba watu hao wahojiwe na wachukuliwe hatua ikibidi,” amesema Selasini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news