NA DIRAMAKINI
JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema kuwa, linaendelea kufanya uchunguzi juu ya tukio la mtoto (jina linahifadhiwa) mwenye umri wa miaka nane ambaye ni mwanafunzi wa Darasa la Tatu Shule ya Msingi Anazak mkazi wa Kimara aliyekutwa amefariki dunia chumbani kwake akiwa amelala.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Muliro J.Muliro akieleza kuwa, tukio hilo limetokea Mei 30, 2022 huko Kimara Temboni katika Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.