NA FRESHA KINASA
MKURUGENZI wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania (HGWT), Rhobi Samwelly ametoa rai kwa Watanzania wote kushiriki kikamilifu kuhesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, mwaka huu. Ili kuiwezesha Serikali kupanga mipango mbalimbali ya maendeleo.

"Asiwepo mtu yeyote atakayeachwa bila kuhesabiwa Agosti 23, mwaka huu. Serikali ina dhamira njema sana ya kuendelea kufikisha Maendeleo kwa wananchi, ili izidi kufanikiwa zaidi lazima iwatambue Watanzania wote. Hivyo sensa ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu,"amesema Rhobi.

Pia, Rhobi amewaomba viongozi wa dini, na wenye nafasi mbalimbali katika jamii kuendelea kutoa elimu kwa wananchi katika maeneo yao juu ya umuhimu wa sensa, kwani jambo hilo ni Muhimu sana lazima liendelee kuzungumzwa mara kwa mara, kusudi siku ikifika Watanzania wote wahesabiwe.