Serikali yadhamiria kutoa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kidigitali nchini

NA OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa amesema Serikali itaimarisha usimamzi wa utaoji wa mikopo ya asilimia 10 kwenye halmashauri kwa kutumia mifumo ya TEHAMA ili mikopo hiyo iweze kuwanufaisha wahusika na kuleta mabadiliko chanya kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Ameyasema hayo leo Juni 24, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha 2022/23 na kueleza kuwa, mfumo wa kielektroniki utasaidia kuongeza usimamizi kwa kutambua anayepewa mkopo, shughulli anayoifanya na urejeshaji wa mkopo katika halmashauri zote nchini.

“Tutasimamia sheria za utoaji wa mikopo ya asilimia 10 na kuhakikiha kila Mkurugenzi anatoa mikopo hiyo kwa wakati na sio kwa hiari bali ni takwa la sheria na kuzingatia utawala bora katika usimamizi wa mikopo hiyo,”amesema Bahungwa.

Bashungwa amesema moja ya kigezo kitakachotumika kupima ufanisi wa Wakurugenzi katika halmashauri ni usimamizi wa utoaji na urejeshaji wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Aidha, Bashungwa amesema Serikali itaimarisha nidhamu katika Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa na kuhakikisha Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa wilaya na Wakurungenzi wa Halmashauri wanatoa ushirikiano kwa Wabunge ambao ni watetezi na wawakirishi wa wanannchi.

Amesema,Ofisi ya Rais-TAMISEMI inaendelea kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zilizopo kwenye baadhi ya halmashauri na kuzipati ufumbuzi wa haraka lengo likiwa ni kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news