NA DIRAMAKINI
SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Geita tarehe 11 Juni,2022 limeendesha Bonanza la Mpira wa Miguu katika Wilaya ya Mbogwe kwa kushirikisha timu mbili za wananchi na timu mbili za shule ya msingi na moja ya sekondari lengo likiwa ni kufikisha elimu ya huduma ya Ni-Konekti.
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Geita, Jaochim Ruweta amefungua bonanza hilo na baadae kukabidhi jezi zenye Nembo ya Ni-Konekt kwa Youth Sport Club na kupokelewa na Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Msingi Mkapa Masumbwe wilayani Mbogwe.
Bonanza hilo liliandaliwa mahsusi kwa ajili ya kufikisha elimu kwa wananchi kuhusu huduma mpya ya Ni-konekt kwa kuwapa maelezo na kutoa ujumbe kupitia fulana .
Baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Ishilanga katika viwanja vya Shule ya Msingi Masumbwe wilayani Mbogwe Mkoa wa Geita waliendelea kupata elimu ya huduma ya Ni-Konekt kutoka kwa wahudumu wa shirika hilo katika uwanja wa shule ya msingi Mkapa mjini Masumbwe.
Afisa Mahusiano wa TANESCO Mkoa wa Geita, Emma Nyaki ameongoza timu ya watumishi wa shirika hilo wanaotoa elimu ya Ni-Konekt wakiwa "Site" wilayani Mbogwe mkoani Geita.