NA MWANDISHI WETU
WAZIRI wa Mambo ya Nje wa Cuba, Mhe. Bruno Rodrieguez Parrilla amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 29 hadi 30 Juni 2022.

Wakati wa mapokezi hayo, Mhe. Balozi mulamula ameeleza madhumuni ya ziara hiyo ni kuimarisha na kukuza ushirikiano wa kihistoria ulioasisiwa na Wasisi wa mataifa hayo mawili, Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere na Hayati Fidel Castor aliyekuwa Rais wa kwanza wa Taifa la Cuba.
Tanzania na Cuba zimeendelea kushirikiana katika maeneo ya afya, elimu, viwanda, na biashara. Pamoja na maeneo hayo serikali hizo mbili zinatarajia kufungua maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Kilimo, utalii, ushirikiano katika usimamizi wa masuala ya zimamoto na uokoaji, utamaduni na michezo.
