TARI, Magereza wadhamiria mambo mazuri katika kilimo

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo nchini (TARI), Dkt.Geoffrey Mkamilo akiongoza wakurugenzi wengine wa TARI, Zephania Mshanga, Dkt.Joel Meliyo na Dkt.Juliana Mwakasendo wametembelea ofisi ya Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Tanzania lililopo Msalato Dodoma.

Lengo likiwa ni kujifunza na kuona shughuli zinazofanywa na jeshi hilo kama hatua za kuelekea kusaini mkataba wa mashirikiano kati ya taasisi hizo mbili.
Dkt.Mkamilo amemhakikishia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee kuwa, TARI ipo tayari kufanya kazi kwa ukaribu na Jeshi la Mageraza kwenye masuala mbalimbali kama uzalishaji wa mbegu, utafiti, usambazaji wa teknolojia za kilimo.

Aidha, Dkt.Mkamilo amelipongeza Jeshi la Magereza kwa kazi nzuri wanazofanya hasa upande wa kilimo mfano uzalishaji wa miche ya michikichi Kigoma kupitia Gereza Lakwitanga.
Naye Kamishina Jenerali wa Jeshi la Magereza, Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee amesema, amefurahi kutembelewa na TARI amepata nafasi ya kujifunza shughuli zinazofanywa na TARI na ameahidi kuendelea kushirikiana ili kulima kwa kufuata ushauri wa kitaalam.

Lengo likiwa ni kuwezesha kilimo kiwe na tija na hivyo kuongeza uzalishaji jambo ambalo litawezesha jeshi kujitegemea.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news