TBA yakabidhi nyumba makazi ya Jaji Mfawidhi Tabora

NA AMANI MTINANGI-Mahakama

WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) imeikabidhi Mahakama ya Tanzania jengo la ghorofa moja na la kisasa kwa ajili ya makazi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora.
Muonekano wa mbele wa jengo la makazi ya Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora.

Hafla ya kukabidhi jengo hilo ambalo limegharimu zaidi ya shilingi milioni 525 za Kitanzania ilifanyika hivi karibuni mjini hapa mara baada ya kukamilika kwa mradi ambao umetekelezwa kwa takribani miaka 10.
Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Tabora, Bw. Ginaweda Nashon (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa TBA Tabora, Bw. Abraham Ndazi wakati wa makabidhiano ya jengo la makazi ya Jaji Mfawidhi lililogharimu kiasi cha zaidi ya shilingi 525.

Kaimu Meneja wa TBA mkoani Tabora, Bw. Abraham Ndazi alikabidhi jengo hilo kwa niaba ya uongozi wa Wakala wa Majengo nchini kwa Kaimu Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Tabora, Bw. Ginaweda Nashon.

Akizungumza katika hafla hiyo, Bw. Nashon alisema kuwa licha ya kumwezesha Jaji Mfawidhi kuishi katika makazi bora na salama, jengo hilo jipya lenye vyumba vitatu pia litapunguza gharama za matumizi ya ofisi.
Kaimu Meneja wa TBA mkoa wa Tabora akiambatana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora, Mhe. Gabriel Ngaeje pamoja na baadhi ya maafisa na watumishi wa Mahakama kukagua jengo hilo wakati wa makabidhiano.

Bw. Nashon ambaye alipokea jengo hilo kwa niaba ya Mahakama ya Tanzania alisema kuwa Mahakama imekuwa ikitumia fedha nyingi kulipia pango la nyumba ya makazi ya Jaji Mfawidhi.

Amesema kiasi cha shilingi milioni 14 za Kitanzania zimelipwa, sawa na shiingi 1,180,000/= kwa mwaka. Bw. Nashon ameupongeza uongozi wa TBA Mkoa wa Tabora kwa kazi nzuri waliyoifanya ya ujenzi hadi kukamilika kwa mradi huo.
Picha ya pamoja baada ya makabidhiano.Naye Kaimu Meneja wa Mkoa wa Tabora aliishukuru Mahakama Kuu Tabora kwa namna wanavyoshirikiana kutekeleza miradi inayosimamiwa na Wakala na kuahidi kuendeleza ushirikiano na Mahakama katika kutekeleza mjukumu yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news