NA DIRAMAKINI
WAZEE wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Vijana na Wadau mbalimbali visiwani Zanzibar wamepongeza hatua ya Mzee Baraka Shamte kuomba radhi CCM pamoja na Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa kauli za kashfa alizozitoa hivi karibuni.

"Mzee Mwenzetu amekosea na amekiri kosa hivyo Mamlaka inapaswa kumsamehe kwa Mujibu wa Kanuni na Taratibu," Wamesema baadhi wazee hao.