NA GODFREY NNKO
LEO Dola ya Singapore (SGD) inanunuliwa kwa shilingi 1664.3 na kuuzwa kwa shilingi 1680.3 huku Krona ya Sweden (SEK) ikinunuliwa kwa shilingi 234.14 na kuuzwa kwa shilingi 236.41.
Picha na Bloomberg.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Juni 10, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Randi ya Afrika Kusini (ZAR) ikinunuliwa kwa shilingi 149.64 na kuuzwa kwa shilingi 150.99 huku dola ya Marekani (USD) ikinunuliwa kwa shilingi 2290.22 na kuuzwa kwa shilingi 2313.12.
Dinar ya Algeria (DZD) inanunuliwa kwa shilingi 16.9 na kuuzwa kwa shilingi 17.0 huku Franka ya Ufaransa (FRF) ikinunuliwa kwa shilingi 308.29 na kuuzwa 311.02.
Lira ya Italia (ITL) inanunuliwa kwa shilingi 1.044 na kuuzwa kwa shilingi 1.054 huku Rupia ya India (INR) ikinunuliwa kwa shilingi 29.47 na kuuzwa kwa shilingi 29.74.
Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 10.86 na kuuzwa kwa shilingi 11.52.
Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.57 na kuuzwa kwa shilingi 19.74 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2462.44 na kuuzwa kwa shilingi 2487.99.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.59 na kuuzwa kwa shilingi 0.62 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.13 na kuuzwa kwa shilingi 50.57.
Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.82 na kuuzwa kwa shilingi 1.84 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7480.7 na kuuzwa kwa shilingi 7545.2.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 343.8 na kuuzwa kwa shilingi 347.2 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.11 na kuuzwa kwa shilingi 17.28.
Dirham ya Umoja wa Falme za Kiarabu (AED) inanunuliwa kwa shilingi 623.6 na kuuzwa kwa shilingi 629.7 huku Schilling ya Australia (ATS) ikinunuliwa kwa shilingi 146.9 na kuuzwa kwa shilingi 148.3.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Fedha za Kigeni
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania
Uchumi na Biashara