NA GODFREY NNKO
LEO Kwacha ya Malawi (MWK) inanunuliwa kwa shilingi 2.08 na kuuzwa kwa shilingi 2.23 huku Rupia ya Pakistan (PKR) ikinunuliwa kwa shilingi 11.02 na kuuzwa kwa shilingi 11.68.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Juni 2, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,Lira ya Italia (ITL) inanunuliwa kwa shilingi 1.044 na kuuzwa kwa shilingi 1.053 huku Rupia ya India (INR) ikinunuliwa kwa shilingi 29.56 na kuuzwa kwa shilingi 29.8.
Shilingi ya Kenya (KES) inanunuliwa kwa shilingi 19.6 na kuuzwa kwa shilingi 19.8 huku Euro ya Ulaya (EUR) ikinunuliwa kwa shilingi 2454.1 na kuuzwa kwa shilingi 2479.6.
Shilingi ya Uganda (UGX) inanunuliwa kwa shilingi 0.58 na kuuzwa kwa shilingi 0.60 huku Franka ya Ubelgiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.11 na kuuzwa kwa shilingi 50.56.
Aidha,Won ya Korea Kusini (KRW) inanunuliwa kwa shilingi 1.84 na kuuzwa kwa shilingi 1.86 huku Dinar ya Kuwait (KWD) ikinunuliwa kwa shilingi 7484.4 na kuuzwa kwa shilingi 7548.9.
Yuan ya China (CNY) inanunuliwa kwa shilingi 343.12 na kuuzwa kwa shilingi 346.42 huku Yen ya Japan (JPY) ikinunuliwa kwa shilingi 17.8 na kuuzwa kwa shilingi 17.9.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Fedha za Kigeni
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania