NA DIRAMAKINI
UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania nchini Malawi umesema kuwa, Serikali ya Malawi imesitisha kuuzwa kwa mahindi nje ya nchi kutokana na mashaka ya kuwa na upungufu wa chakula.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi, Mheshimiwa Humphrey Polepole kwenda kwa wafanyabiashara wa mazao hapa nchini.
Balozi Polepole amesema Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malawi unafuatilia suala hilo kwa karibu huku ukiwataka wafanyabiashara kusitisha mpango wa kununua mahindi nchini Malawi mpaka Ubalozi utakapotoa taarifa nyingine.