Watoto wenye ulemavu wana haki, ndoto zao tuwape elimu wasema Wadau

NA SHEILA KATIKULA

JAMII imeombwa kuwalinda na kuwatetea watoto wenye ulemavu mbalimbali kwa kuwapa elimu bora ili waweze kutumiza ndoto zao.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wanaharakati wa kutetea haki za watoto hao wamesema jamii imeshindwa kutimiza wajibu wao kwa watoto na kupelekea kuwaficha ndani kwa sababu ya ulemavu kufanya hivyo ni kosa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Beyond Giving linalojishughulisha na watoto wenye ulemavu,Joseph Msuka amesema, lengo la shirika hilo ni kuhakikisha wanalinda,kusaidia na kutetea haki za watoto wenye ulemavu ili waweze kupewa elimu bora na wasifanyiwe vitendo vya ukatili na kwani mpaka hivi sasa kituo hicho kina watoto 60 ambao wanatoka kwenye wilaya za Magu,Ilemela na Nyamagana.

"Tumesaidia watoto zaidi ya 100 kwa kuwapa elimu bora na kuhakikisha wanapata huduma za matibabu kwa kuwakatia bima za afya na kuwapa mahitaji muhimu.

"Naiomba jamii itambue kuwa watoto wenye ulemavu wanahaki ya kupata elimu kama wengine na siyo kuwaficha ndani kwani kufanya hivyo ni kosa.
"Inaskitisha kuona baadhi ya wanaume hutelekeza familia zao kwa sababu ya kupata mtoto mwenye ulemavu na kupelekea kulelewa na mzazi mmoja ni vema kila mtu kushiriki katika makuzi na malezi ya watoto wao,"amesema Msuka.

Naye mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Railway Children Africa (RCA) linalojishughulisha na watoto wanaoishi na kufanya kazi mtaani, Judith Kasera amesema wanafanya kazi kwa kushirikiana na Serikali kwa kusimamia Sheria ya Mtoto ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 sanjari na kuwarudisha watoto hao kwa wazazi wao ili waweze kupata malezi ya wazazi wao.

"Shirika letu lina kitengo cha kusimamia ulinzi na usalama wa watoto na tunahakikisha watoto wanaopitia vitendo vya ukatili wanaripoti kesi zao ili kuweza kupata ufumbuzi,"amesema Kasera.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Action for Community Development (ACODE),Winner Chimba amesema, watoto wenye mtindio wa ubongo hukosa malezi kwa familia zao tofauti na wenye ulemavu wa viungo. 

Hata hivyo, ameongeza kuwa jukumu la kuwalinda watoto hao siyo la Serikali bali jamii nzima inawajibu wa kuwalinda,kuwaheshimu na kuwathamini kuwapa elimu na malezi bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Living Together Autistic Foundation (Li-TAFO) inayojishughulisha na watoto wenye usonji, Shangwe Mgaya amesema lengo la taasisi hiyo ni kujenga uelewa kwa jamii kwa kuwaelimisha ili waweze kuona umuhimu wa watoto hao na siyo kuwatelekeza.

Amesema, usonji ni changamoto iliyopo kwenye mfumo wa ufahamu inayopelekea mtoto kushindwa kuwasiliana,kuçhangamana na wengine, kushindwa kuzoea mazingira mapya inayoweza kuharibu hisia na tabia zake.

"Shirika letu baada ya kuona umuhimu wa watoto hawa tumetoa bima za afya kwa watoto 1,000 ili waweze kupata huduma kwa urahisi kutokana na changamoto hiyo.

"Wakati umefikia wazazi kuacha kuwaficha watoto wenye usonji ndani kwa sababu ya changamoto zao, kuona ni mkosi au laana kitu ambacho siyo sahihi watoto hawa wanauelewa mkubwa na wanafundishika kwaiyo jamii inatakiwa iamke na iimarishe ulinzi kwa watoto,"amesema Mgaya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news