Watumishi TRA Mtwara wachunguzwe-Shaka

NA DIRAMAKINI

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuhakikisha wanafuatilia na kuwachukulia hatua baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) mkoani humo.

Ni watumishi ambao wamekuwa sio waadilifu ambao wamekuwa wakitumia nafasi zao kuwanyanyasa wafanyabiashara kwa kuwafungia biashara zao.
Shaka ameyasema hayo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku nne mkoani Mtwara.

"Mkuu wa Mkoa huko TRA kuna mambo inabidi mkayaangaliee, Rais alipoingia madarakani jambo moja kubwa alilolifanya ni kufungua uchumi wa nchi, kuna biashara zilifungiwa Rais alipoingia zikafunguliwa.

"Kuna watu wanafungia watu biashara, lakini TAKUKURU tusaidieni mkitaka tuwasaidie tutawapa baadhi ya watumishi wa TRA vitendo wanavyofanya haviendani na maadili ya kazi zao.

"Kumekuwa na wimbi la kufunga biashara za watu kwa makosa madogo madogo ambayo hayana msingi hatuwezi kuona dhamira njema ya Rais inakwamishwa baadhi ya watu wanataka kumkwamisha Rais Samia,"amesema.


Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news