NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki chini ya uongozi wa Waziri Liberata Mulamula imeendelea kutumia majukwaa ya kimataifa kuitangaza nchi na fursa zake kama sehemu ya utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri Mkuu wa Canada, Mhe Justin Trudeau wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022. Katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaohitimishwa leo tarehe 25 Juni 2022 nchini Rwanda na kuhudhuriwa takribani na viongozi wa kaliba na ngazi tofauti wa nchi zote 54 za umoja huo, Tanzania ilitumia fursa hiyo kuhamasisha wawekezaji na kuja nchini.
Balozi Liberata Mulamula alionekana akifanya mazungumzo rasmi na yasiyo rasmi na Mawaziri wenzake wa Mambo ya Nje na hata Mawaziri Wakuu na Marais wa nchini mbalimbali kwa lengo la kuitangaza nchi. Alisikika akiwaambia, “Rais wetu, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kuboresha mazingira ya biashara, hivyo milango ipo wazi, waambieni wafanyabiashara wenu waje kuwekeza Tanzania kwenye sekta mbalimbali na hasa kilimo ambacho ni moja ya kipaumbele cha Serikali ya awamu ya sita”.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri Mkuu wa Canada, Mhe Justin Trudeau wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022. Mwingine katika picha ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Mélanie Joly.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea jambo na Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea jambo na Rais wa Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea jambo na Rais wa Nigeria, Mhe. Muhammadu Buhari wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025.
Viongozi ambao Mhe. Waziri Mulamula alipata fursa ya kufanya nao mazungumzo rasmi ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore, Mhe. Dkt. Vivian Balakrishnan; Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Subrahmanyam Jaishankar; Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Mhe. Hina Rabbani Khar na Mke wa Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza na Mwanzilishi wa Mfuko wa Cherie Blair, Bibi Cherie Blair.
Viongozi Wakuu aliokutana nao na kuwapa salamu za Rais Samia ni pamoja na Waziri Mkuu wa Canada, Mhe. Justin Trudeau; Rais wa Rwanda, Mhe. Paul Kagame; Rais wa Zambia, Mhe. Hakainde Hichilema; Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta; na Rais wa Nigeria, Mhe. Muhammadu Buhari.
Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine, Balozi Mulamula alihimiza ushirikiano katika biashara na uwekezaji, mafunzo, usafiri wa anga na utalii. Alieleza namna Serikali ya awamu ya sita inavyofanya jitihada kuondoa vikwazo vya kibiashara na kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kushawishi wawekezaji wengi. Aliziomba Canada, Singapore, India na Pakistan kuleta wawekezaji wengi zaidi na hasa katika sekta ya kilimo ambayo ni kipaumbele cha Serikali ya awamu ya sita.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea jambo na Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongozana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango kuingia kwenye ukumbi unaofanyika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore, Dkt. Vivian Balakrishnan wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Singapore, Dkt. Vivian Balakrishnan wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Modola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2025. Balozi Mulmula alitumia fursa pamoja na mambo mengine kuwakaribisha wafanyabiashara wa Singapore kuja kuwekeza Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea jambo na Mkurugenzi wa Afrika katika Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Naimi Aziz. Wengine katika picha ni Maafisa wa Mambo ya Nje, Bi.Talha Waziri (kulia) na Bi. Lilian Mukasa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan, Mhe. Bilawal Bhutto Zardari wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe Subrahmanyam Jaishankar wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula na ujumbe wake wakiwa katika mazungumzo na na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe Subrahmanyam Jaishankar wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022.
Kuhusu utalii, Mhe. Waziri aliziomba nchi hizo kutafsiri Filamu ya The Royal Tour iliyoongozwa na Rais Samia kwa lugha za nchi zao ili iwafikie watu wengi zaidi. Aidha, alizihimiza nchi hizo, hususan India na Singapore kuanzisha safari za moja kwa moja za mashirika yao ya ndege kati ya Tanzania na nchi hizo ili kuhamasisha utalii.
Aidha, Mhe. Waziri alihimiza ushirikiano na Singapore katika Uchumi wa Buluu kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa kwenye eneo hilo, hususan kwenye uendelezaji, usimamizi na uendeshaji wa bandari. Aligusia pia umuhimu wa kujengeana uwezo hususan katika eneo la rasilimali watu na mafunzo ya TEHAMA.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiongea jambo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia, Mhe.Netumbo Nandi-Ndaitwah wakati wakielekea kwenye ukumbi unaofanyika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone, Mhe. Prof. David Francis wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashaiki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Zambia, Mhe. Stanley Kakubo wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola unaofanyika Rwanda tarehe 20 hadi 25 Juni 2022.
Wakati wa mazungumzo na Bibi Cherie Blair, alielezea utayari wa Mfuko wake wa Cherie Blair Foundation wa kushirikiana na Tanzania, kwenye kuwajengea uwezo wanasheria wa kuwa na ujuzi wa kutosha wa upatanishi na usuluhishi wa migogoro nje ya mahakama na kwamba mfuko huo pia, upo tayari kuisaidia Tanzania kwa kutoa msaada kwa mawakili katika kesi za Kimataifa zinazoikabili Serikali ya Tanzania.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Madola utafungwa leo jioni na Balozi Mulamula ataendeelea na mkakati wake wa kukutana na viongozi mbalimbali na atarejea nchini tarehe 26 Juni 2022.