*Asisitiza maoni ya wadau kuhusu mapitio ya Sera ya Elimu, Mitaala ya Elimu yatapewa kipaumbele
NA MATHIAS CANAL-WEST
SERIKALI imesema itachukua na kuyafanyia kazi maoni yote yanayotolewa na wadau wa elimu kuhusu Mapitio ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 na mitaala ya elimu ili kufanya mageuzi makubwa ya elimu nchini yanayotarajiwa kufanyiwa maamuzi mwakani.


Utekelezaji wa programu hiyo utakuwa wa miaka mitano kuanzia mwaka huu 2021/2022 hadi mwaka 2025/2026 na ina thamani ya Dola za Kimarekani milioni 500 ambazo ni sawa na takribani shilingi trilioni 1.15 za kitanzania. "Afua zote nane nilizozitaja zitatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo".

Aidha, amesema kuwa baadhi ya shughuli zitatekelezwa na Taasisi za kielimu zikiwemo Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), Tume ya Utumishi ya Walimu (TSC) na Mamlaka za Serikali za Mitaa huku baadhi ya Wizara zikishirikishwa katika utekelezaji wa afua zinazoendana na kazi za msingi za Wizara husika.
Waziri Mkenda ameyataja Matokeo yanayotarajiwa kupatikana katika miaka mitano ya utekelezaji wa programu hiyo kuwa ni pamoja na Vyumba vya madarasa 12,000 kujengwa ambapo lengo ni kujenga angalau vyumba vya madarasa 3,000 kila mwaka kuanzia mwaka ujao wa fedha 2022/2023,
Ameyataja matokeo mengine kuwa ni pamoja na uandikishaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali kuongezeka; Kuimarika kwa utawala na usimamizi wa shule katika ngazi ya shule na kata; na Kuimarika kwa ubora na uwezo wa walimu katika ufundishaji kutokana na mafunzo ya walimu kazini.