NA DIRAMAKINI
WAZIRI wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Nape Nnauye ameshiriki Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika (International Day of the African Child) kwa kukabidhi vifaa vya TEHAMA vilivyotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ( UCSAF) katika Shule ya Sekondari Chinangali, Mkoani Dodoma.

"Ni matumaini yetu vifaa hivi vitatumika kuongeza uwezo wa utoaji wa huduma za elimu katika shule yetu, ninaamini kuwa ufaulu utaongezeka na uwezo wenu wa kukabili mazingira pia utaongezeka,"aliongeza Waziri Nnauye.

Kwa upande wake, Kaimu Mtendaji Mkuu wa UCSAF John Munkondya amesema, UCSAF imetoa komputa tano kwa shule hiyo ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa mradi wa kuzipatia shule za umma vifaa vya TEHAMA na kuziangusha na mtandao wa intaneti.

Pia ameahidi kuwa taasisi hiyo itahakikisha kuwa walimu katika shule ya Sekondari Chinangali wanapatiwa mafunzo ya matumizi bora ya vifaa hivyo ili viweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
"Baada ya kukabidhi vifaa hivi tunaomba walimu wataochaguliwa waingie katika mpango wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu kwa mwaka wa Fedha 2022/2023".
