GENEVA-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako ameongoza ujumbe wa nchi katika Mkutano wa 110 wa Kazi wa Kimataifa leo Juni 7, 2022 jijini Geneva, Uswisi.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgCaAJnBqFeERRB8XjuiRG1OjAQaQDPLwyorntClUqO9QMguB0LI-eE4tp2kamEtBAXGtB5UTQOvVG-L0Y1kft0CqaLytwk3ZlecAGP09DS0A1-X_dTU-3dzXOPB-0UvoI0Rsvpep_62Y7LeEqbM-7r7yYaHOn9-qi-FHugxGswif8z6LeQvQ/s16000/C1.jpg)
Pia Waziri Ndalichako ameshiriki pia kikao cha kundi la
Afrika ambapo ametoa salamu za nchi na kuwaalika nchi wanachama wa
Afrika na duniani kote kutembelea nchi ya Tanzania kwa lengo kujionea
vivutio vya kitalii na shughuli za ustawi wa wananchi zinazotekelezwa
vizuri na Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.