NA ROTARY HAULE
WIZARA ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa (UNESCO) wameungana kwa pamoja katika kikao kazi cha ushauri kwa ajili ya uimarishaji wa Matokeo ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari hapa nchini.

Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Maelezo, Patrick Kipangula.
Akizungumza mara baada ya ufunguzi wa kikao hicho, Mkurugenzi Msaidizi wa Habari Maelezo, Patrick Kipangula amesema kuwa, kikao hicho cha siku tano kinalenga kuimarisha na kuweka vipaumbele katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSCDF).
Kipangula amesema kuwa, mpango huo ulizinduliwa Mei 17, mwaka huu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Philip Mpango ambao utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia 2022 hadi 2027.
Aidha, Kipangula amesema mpango huo unafafanua na kufanikisha ajenda ya Taifa ya Maendeleo na Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)ili kuthibitisha hatua za kipaumbele kwa maendeleo ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.
Kipangula ameongeza kuwa, kikao kinachofanyika hivi sasa Wilayani Bagamoyo kinatumika kujenga uelewa kwa Serikali,Umoja wa Mataifa na wafadhili na kubadilishana kwa ushirikiano juu ya hatua zilizopangwa ndani ya mfumo wa UNSCDF.

Kipangula, amesema pamoja na lengo kuu lakini yapo malengo mahususi ikiwemo kuoanisha wahusika wakuu katika vipaumbele vya Serikali na dira ya mchango wa kisekta kwenye mfumo wa Maendeleo ya Ushirikiano Endelevu wa Umoja wa Mataifa (UNSCDF).
Ametaja malengo mengine kuwa, ni kuweka mikakati yenye mwelekeo wa matokeo shirikishi na mipango ya kuimarisha mchango wa Sekta katika maendeleo endelevu na masuala mengine yanayohusiana.

Angulo,amesema programu hiyo italenga katika maendeleo ya habari,usalama kwa Waandishi wa habari,nafasi ya Waandishi katika kukuza maendeleo ya nchi na masuala ya Wanawake.
Hata hivyo,Angulo ametaja maeneo mengine yatakayoguswa ni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi (Climate Change), Ukatili wa Wanawake na Watoto,Demokrasia na uchaguzi.