NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Madini inaendelea na mafunzo ya ununuzi na ugavi kwa Idara na Vitengo vyake.
Mafunzo hayo yametolewa kwa Idara na Vitengo leo Juni 21, 2022 ambapo yamehusisha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) na Kitengo cha TEHAMA (ICT) katika ukumbi wa wizara jijini Dodoma.
Katika mafunzo hayo, watumishi wanapatiwa mafunzo ya taratibu za ununuzi kuanzia kwa mtumiaji hadi katika Kitengo cha Menejimenti ya Usimamizi wa Ununuzi (PMU) kwa mujibu wa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016.
Pia, yatatolewa mafunzo kuhusu mpango wa manunuzi ya Wizara ya Madini unaotokana na bajeti ya kila mwaka.
Aidha, mafunzo kuhusu utaratibu wa utoaji mafuta na mifumo ya mafuta ya GPSA na mfumo wa wizara.
Zifuatazo ni picha za mafunzo hayo kwa kitengo cha GCU na ICT;