NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amesema Wizara ya Maliasili na Utalii iko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau wanaofanya jitihada za kuunga mkono juhudi za Serikali kwa kuandaa matamasha ya kutangaza utalii wa utamaduni na malikale.