Zifahamu hatua za Maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022

NA DIRAMAKINI

KWA mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi hufanyika katika awamu kuu tatu ambazo ni Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu, Wakati wa Kuhesabu Watu na Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu.
Kipindi Kabla ya Kuhesabu Watu

Kipindi kabla ya kuhesabu watu kinajumuisha Uandaaji wa Kitabu cha Mkakati wa Usimamizi na Utekelezaji wa Sensa na nyaraka nyingine, Utengaji wa Maeneo ya Kuhesabia Watu na Uzalishaji wa Ramani, Uandaaji wa Nyenzo (Madodoso na Miongozo mbalimbali).

Kipindi cha Kuhesabu Watu

Kipindi cha kuhesabu watu kinajumuisha kazi kuu na muhimu katika zoezi hili ya kuhesabu watu.

Kipindi Baada ya Kuhesabu Watu

Kipindi baada ya kuhesabu watu kinajumuisha Uchakataji wa Taarifa za Sensa, Uchambuzi, Utoaji wa Matokeo ya Awali, Usambazaji wa matokeo ya mwisho, uhamasishaji wa matumizi ya takwimu kwa watumishi wa wizara, idara na taasisi za Serikali.

Aidha, maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi 2022 yalianza 2018, ikiwa ni kutenga maeneo ya kuhesabia watu, kutayarisha nyaraka muhimu za sensa kama vile madodoso, miongozo, fomu za kudhibiti ubora na kufanya sensa ya majaribio. #JIANDAEKUHESABIWANIAGOSTI23

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news