Balozi Kattanga atembelea banda la Mahakama ya Tanzania Maonesho ya Sabasaba

NA MWANDISHI WETU 

KATIBU Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga amefanya ziara na kutembelea banda la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl. Nyerere jijini Dar es salaam na kushuhudia huduma mbalimbali zinazoendelea kutolewa na Mahakama kwa wananchi.

Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akitia sahihi kwenye kitabu cha wageni wakati huo akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Kumbukumbu za Utawala Mahakama ya Tanzania, Bw. Daniel Msangi (kushoto) alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam, Julai 6, 2022.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga (mwenye kaunda suti ya bluu) alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akipokea zawadi ya vitabu na machapisho mbalimbali kutoka kwa Muhadhiri wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Dkt. Kevin Mandopi alipowasili kwenye Banda la Mahakama ya Tanzania kukagua huduma mbalimbali zinazotolewa na Mahakama katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga akipewa maelezo kutoka Kiongozi wa Kituo cha Huduma Kwa Mteja cha Mahakama, Bi. Evetha Mboya (aliyenyoosha mikono) ya namna kituo hicho kinavyotoa huduma zake kwenye katika Maonesho ya 46 ya Sabasaba katika Viwanja vya Mwl. Nyerere Jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi Hussein Kattanga (aliyenyoosha kidole) akitoa maelekezo kwa mtoa huduma (hayupo pichani) wakati alipotemebelea Banda hilo.(Picha na Innocent Kansha-Mahakama).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news