NA DIRAMAKINI
KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Bw.Fadhil Fabian Ngajilo leo amejitosa kuchukua fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania nafasi ya Uwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi mkoani hapa.

Kada huyo aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa kati ya mwaka 2008 hadi 2012.

Bw.Ngajilo mbali na kujihusisha katika siasa mkoani Iringa pia ni miongoni mwa wadau muhimu wa maendeleo ambao mara kwa mara amekuwa akishiriki shughuli za maendeleo ikiwemo kijamii, kiuchumi na michezo.