DARAJA JIPYA WAMI:Septemba 1, Watanzania kufurahia matunda ya kodi zao

NA DIRAMAKINI

UJENZI wa Daraja jipya la Wami lililopo Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani umefikia asilimia 93 na unatarajiwa kukamilika Agosti 31, mwaka huu.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhandisi Godfrey alipotembelea kukagua ujenzi wa Daraja hilo mradi huo unajengwa na kampuni ya Power Construction Corporation of China Ltd ikisimamiwa na kampuni ya Ilshin Engineers and Advance Solutions Ltd ya Tanzania na limegharimu kiasi cha shilingi bilioni 75.1
Kasekenya alisema kuwa daraja hilo limeghatimu nchi fedha nyingi kwani limwjengwa kutumia teknolojia ya kisasa ambalo lina urefu wa mita 510 likiwa na barabara unganishi kutoka kila upande zenye urefu wa kilometa 3.8 zikiwa zimefikia asilimia 73.

"Ujenzi tumeambiwa unakamilika mwishoni mwa mwezi huu Agosti 31 na tunatarajia magari yaanze kupita Septemba Mosi, mwaka huu na litasaidia kupunguza ajali zilizokuwa zikitokea kwenye daraja la zamani ambalo lilijengwa mwaka 1959,"alisema Kasekenya.

Alisema kuwa ujenzi wa miundombinu unaendelea ambapo serikali ya awamu ya sita inaendelea kusimamia na kutoa fedha kwa ajili hiyo lengo likiwa ni kuifanya nchi kuwa na miundombinu mizuri.

"Kupitia ujenzi wa Daraja hili wataalamu wa hapa nchini wamejifunza teknolojia mpya ambapo asilimia 91 ni wataalamu wa ndani na asilimia tisa ni kutoka nje ya nchi mbali ya kupata utaalamu pia wamejiongezea kipato kupitia mradi huo,"alisema Kasekenya.

Aidha alisema kuwa malengo ya ujenzi wa Daraja hilo ni kukabiliana na changamoto ya ajali, kutumia muda mwingi, uharibu wa mali kutokana na daraja hilo kuwa jembamba na kona kali.

"Hichi ni kielelezo cha Rais bora wa kusimamia miundombinu na haya yalimfanya ateuliwe na bado anaendelea kutuonyesha ujenzi wa miundombinu bora,"alisema Kasekenya.

Naye Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Pwani Baraka Mwambage alisema kuwa lengo la kujenga daraja hilo ni kutatua changamoto zitokanazo na daraja la zamani ambalo halikidhi mahitaji kwani ni jembamba lenye njia moja.

Mwambage alisema kuwa ujenzi huo umetumia Teknolojia ya madaraja marefu na litakuwa na taa za mionzi ya jua zenye kamera 78 ambapo fidia za mali zilizotolewa ni milioni 194.7. Mradi huo ulianza mwaka 2016.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news