NA DIRAMAKINI
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga,Dkt.Mshindo Msolla amesema,akistaafu Jumapili ya wiki hii katika nafasi hiyo ya uwenyekiti ataendelea na ajenda zake mbili.
MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga,Dkt.Mshindo Msolla amesema,akistaafu Jumapili ya wiki hii katika nafasi hiyo ya uwenyekiti ataendelea na ajenda zake mbili.

"Mimi binafsi nitaendelea na ajenda kuu mbili baada ya kustaafu Jumapili, la kwanza nitahamasisha umoja nchi nzima na la pili nitaendelea kuhamasisha mashabiki wetu waendelee na usajili.
"Aliyechukua fomu ya Urais ana uwezo mkubwa wa kuendeleza kile ambacho tulikianzisha, nitaendelea kumuunga mkono na kuzunguka nchi nzima na wenzangu kuhamasisha umoja wa klabu yetu,"amesema Dkt.Msolla