Tangu Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan iingie madarakani, kuna mabadiliko makubwa yamefanyika katika sekta ya uwekezaji, hatua ambayo imefungua milango kwa wawekezaji wa ndani na nje kuwekeza mitaji yao katika miradi mbalimbali nchini.