Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo Julai 28,2022



















Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Tanzania limepiga marufuku matumizi na kuifutia usajili dawa ya Hensha maarufu mkongo inayomilikiwa na kituo cha Nyasosi Traditional Clinic cha jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa Julai 27, 2022 mjini Morogoro na Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Hamis Malepo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Pia, baraza hilo limekitaka kituo hicho kuhakikisha kinaiondoa sokoni mara moja dawa hiyo ya mkongo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mmiliki wa kituo hicho.

Profesa Malebo amesema hivi karibuni baraza lilifanya uchunguzi wa dawa za tiba zilizo sokoni (Post Market Surveillance) katika maeneo mbalimbali nchini na kubaini kuwepo kwa mapungufu madogo hasa kwenye uandishi wa lebo na vifungashio.

Amesema dawa mbili zilibainika zimesibikwa na vimelea ambavyo ni kiashiria cha hali duni ya usafi wa mazingira ya kutengenezea dawa.

Amesema baraza lilibaini dawa iitwayo Hensha maarufu Mkongo ilikutwa imechanganywa na dawa iitwayo Slidenafil kwa jina maarufu la biashara Viagra ama Erector kitendo ambacho ni kinyume cha sheria na miongozo ya usajili wa dawa za tiba asili na mbadala.

Mwenyekiti huyo amesema mganga ambaye anahitaji kutangaza dawa yake ni lazima afuate utaratibu wa kusajili dawa kwa kupima ubora, usalama na baade kuomba kibali cha matangazo kutoka baraza.

“Kutangaza dawa na huduma ya tiba asili na tiba mbadala bila ya kuwa na usajili na ithibati ya baraza ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) cha kanuni ya dawa asili ya mwaka 2008,” amesema.

Profesa Malebo amesema Baraza lina wajibu wa kuziondoa dawa ambazo usalama na ubora wake haupo katika viwango sahihi kama ilivyobainishwa kwenye kifungu cha 13(1) cha kanuni ya dawa asili ya mwaka 2008.

Mwemyekiti huyo amewataka wananchi pamoja na kutumia tiba lishe zinazoboresha afya kuzingatia taratibu na kanuni za afya ili kujikinga na maradhi ya aina mbalimbali.

Mkazi wa manispaa ya Morogoro, Juvenalius Mkude amelipongeza baraza hilo ya kufungia dawa hiyo kwani imekuwa ikitumika kiholela na watu wengi hususani vijana kwa nia ya kuongeza nguvu za kiume.

“Hiyo dawa binafsi siipendi inadhalilisha wanaume, wengi wetu sasa tumekuwa hatutumii vyakula asili ama sawa asili zinazotambulika, kalini kikubwa zaidi ni namna hata hawa waganga wetu wanavyotuharibu kwa kutuchanganyia dawa asili na dawa nyingine,”alisema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news