Hamasa yashika kasi kila kona,Kamisaa wa Sensa atoa neno Katavi

NA DIRAMAKINI

WANANCHI wote walioomba nafasi ya kuwa Makarani na Wasimamizi wa Maudhui na Maofisa TEHAMA wametakiwa kuwa na subira kuhusu kutangazwa kwa majina ya watahimiwa watakaoshiriki kwenye usaili wa nafasi husika kwenye utekelezaji wa Sensa.
Wito huo umetolewa na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022, Mhe. Anne Makinda alipokutana na Kamati ya Sensa ya Mkoa wa Katavi pamoja na Wadau wa Maendeleo wa mkoa huo.
Mama Makinda amesema, Sensa ina ratiba yake ambayo inatambulika Kimataifa na hivyo kila kitu kinafanyika kwa wakati.

“Kuna watu wananung’unika kwanini hatutoi majina ya waliochaguliwa kuwa Makarani na Wasimamizi wa Sensa, Ofisi za Takwimu zinafuata utaratibu wa Kitaifa na Kimataifa na kuna ratiba yake ya kutekeleza Sensa,”amesema Makinda.
Amesema kwa sasa mafunzo ya Wakufunzi ambao watafundisha Makarani wa Sensa ndio yanaendelea na yakikamilika yatafuata mafunzo ya Makarani na Wasimamizi wa Maudhui.

Sensa ya Watu na Makazi itafanyika tarehe 23 Agosti, 2022. Sensa kwa Maendeleo, Jiandae Kuhesabiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news