NA OR-TAMISEMI
UJUMUISHAJI wa shule hii unaonekana katika mchakato wa kutambua na kujibu utofauti wa mahitaji ya wanafunzi wote kupitia ushiriki mkubwa katika ujifunzaji, tamaduni na jamii, na kupunguza kutengwa katika elimu.
Shule hii ni ya kwanza Tanzania inayojibu maswali mengi ya Elimujumuishi iliyojengwa na Serikali kupitia Mradi wa Lipa kulingana na matokeo (EP4R) na inazinduliwa rasmi leo na Naibu Waziri Elimu, Mheshimiwa Omary Kipanga.
Hapo awali watoto wenye mahitaji maalum walipelekwa kwenye shule za kawaida ambapo kwa namna moja ama nyingine walipata changamoto kadha wa kadha katika kupata elimu yao.
Ndipo Serikali ilipochukia hatua ya kujenga shule hii ya mfano ambayo ni jumuishi yenye mazingira wezeshi, walimu maalum, vitabu na miundombinu yote inayohakisi mahitaji ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Serikali imewachukulia wanafunzi wenye mahitaji maalum kuwa sehemu ya mfumo, kujali tofauti na kuweka mfumo unaokidhi mahitaji ya kielimu ya kila mtoto Ili wote, bila kujali changamoto walizonazo, waweze kujifunza kwa usawa.
Elimu jumuishi inataka kufanikisha ujifunzaji mzuri kwa watoto wote na vijana, kila wakati inalenga kushinda tofauti na kutengwa, kutoka kwa mtazamo wa kibinadamu.