NA MWANDISHI WETU
WANANCHI na Wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wamefurahishwa na uboreshwaji wa huduma za Mfuko huo ambazo kwa sasa zinapatikana kwa njia ya kielekroniki.
Hayo wameyasema kwa nyakati tofauti katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara Sabasaba yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Akizungumzia kuridhishwa kwa huduma hizo, Bw. Andrew Elias ambaye alifika katika banda la NHIF kwa lengo la kupata huduma ya elimu na kujiunga na huduma za Mfuko.
Akizungumzia ushiriki wa Mfuko katika Maonesho hayo, Meneja Uhusiano wa NHIF, Bi. Anjela Mziray alisema kuwa, Mfuko umejipanga kurahisisha zaidi huduma kupitia mitandao kutoa huduma bora na za haraka kwa wananchi lakini pia kuhamasisha wajiunge na huduma ili wawe na uhakika wa matibabu wakati wowote.