NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, IJP Camilius Wambura amewaomba wananchi hususani wakazi wa Jiji la Arusha kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na wale wote wenye nia ya kuchafua taswira nzuri ya nchi na jiji la Arusha.
IJP Wambura amesema Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha amani na utulivu unakuwa wa kutosha ikiwa ni pamoja na viongozi mbalimbali wanaofika nchini Tanzania.