IMF yaidhinisha trilioni 2.5/- mkopo nafuu kwa Tanzania

NA DIRAMAKINI

BODI ya Wakurugenzi ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) imeidhinisha mkopo nafuu wa Dola za Marekani Bilioni 1.05 (zaidi ya trilioni 2.5) kwa ajili ya kuimarisha uchumi wa Tanzania.

Sambamba na kukabiliana na madhara ya kiuchumi ambayo yametokana na vita vya Urusi na Ukarine, fedha zinazotolewa ndani ya miezi 40 kupitia Mpango wa Nyongeza ya Mikopo (ECF) huku wakitanguliza dola milioni 151.7.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Julai 18,2022 na IMF pia fedha hizo zinalenga kujenga uchumi himilivu na kusaidia mageuzi ya kimuundo yatakayoleta ukuaji wa uchumi jumuishi kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya Tanzania.

"Mageuzi yatazingatia kuimarisha nafasi ya kifedha kwa matumizi ya kijamii yanayohitajika sana na uwekezaji wa umma wenye matokeo mazuri,kimuundo na kimamlaka na kuimarisha utulivu wa kifedha,"imeeleza IMF.

Mpango wa Nyongeza ya Mikopo (ECF), ikiwa ni sawa na uwiano wa 795.58 wa Haki Maalum au asilimia 200 ya mgawo wa nchi, au hisa za IMF, kwa Tanzania unafuatia usaidizi wa dharura wa IMF wa dola milioni 561.5 mwaka 2021.

Hazina hiyo ya IMF inalenga kubadilisha mikopo ya usaidizi ya hali ya chini ya UVIKO-19 kuwa ya muda mrefu.

IMF imesema mpango huo mpya unatarajiwa kuchochea msaada wa ziada wa kifedha ili kusaidia kuvutia uwekezaji katika sekta binafsi.

Kwa mujibu wa taarifa ya IMF,vita vya Ukraine ilikuwa ikikwamisha ahueni ya kujikwamua taratibu kwa Tanzania kutokana na janga la UVIKO-19.

"Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa za maendeleo ikiwa ni pamoja na makovu yanayotokana na COVID-19 na vita vya Ukraine, ambavyo vina hatari ya kumomonyoa mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana kwa bidii,"ameeleza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IMF, Bo Li katika taarifa ya IMF.

Awali, IMF ilitoa zaidi ya shilingi trilioni moja kwa Tanzania kutoka mfuko wa mkopo wa dharura, lengo likiwa ni kusaidia juhudi za serikali za kukabiliana na uhitaji wa dharura katika sekta ya afya, misaada ya kibinadamu na changamoto nyingine za kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news