Jukumu lililofanywa na Askari Mashujaa wa Afrika (Operesheni Dragoon) katika Jeshi la Ufaransa wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia lilivyosahaulika duniani

NA CHARLES REGASIAN

OPERESHENI Dragoon mwanzoni ilikuwa ifanyike siku ya mashambulizi makubwa dhidi ya vikosi vya Ujerumani wakati wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (1939-1945)

Dragoon ilifanyika miaka 75 iliyopita ili kuikomboa Ufaransa. Operesheni hiyo Ilihusisha majeshi ya Muungano kutoka mataifa ya Ufaransa, Marekani, Canada na vikosi vya Uingereza.

Operesheni hiyo ilisaidia kukomesha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na wanajeshi wengi wa Afrika walishiriki vita hivyo.
Operesheni hiyo ilifanyika siku ambayo majeshi ya Ufaransa na washirika wake walivishambulia vikosi vya Ujerumani iliyokuwa chini ya utawala wa kidikteta wa Adolph Hitler.

Agosti 15, miezi miwili baada ya moja ya mgogoro mkubwa wa kivita kutokea duniani wanajeshi toka Afrika walichukuliwa na Ufaransa kutoka sehemu mbali mbali katika juhudi ya kuisaidia nchi hiyo kukabiliana na uvamizi wa wanajeshi wa Ujerumani.

Jina lake la siri liliitwa ''Operation Dragoon'' na ukumbusho wake mpaka leo unasherehekewa kila mwaka na viongozi wa mataifa ya Afrika,kila mwaka Rais wa Ufaransa huwaalika marais wa Ivory Coast na Gunea.

Wanajeshi wa Algeria walionekana katika picha kadhaa duniani wakiwachunga wafungwa wa kivita wa Ujerumani wakati wa Operasheni ya Dragoon.

Wanajeshi kutoka makoloni ya Ufaransa ya Kiafrika walichangia theluthi mbili ya jeshi la Ufaransa mwaka 1944, baada ya taifa hilo kupata hasara kubwa kwa kuvamiwa na Ujerumani mwaka 1940.

Wanajeshi wa (Kifaransa) waliotua Kusini mwa Ufaransa walitoka mataifa ya Kaskazini mwa Afrika, Inakadiriwa kuwa zaidi ya wanajeshi milioni moja wa Kiafrika walishiriki Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Awali ilipangwa kufanywa siku muhimu ya kuikomboa Ulaya kutoka kwa Wanazi wa Ujerumani Kaskazini mwa Ufaransa iwe Juni tarehe sita mwaka 1944, na Operesheni ya Dragoon ilifutiliwa mbali kwa kukosa nguvu kazi.

Hata hivyo, mkakati wa kuwarudisha nyuma wanajeshi wa Ujerumani ulikwama. Lengo lilikuwa kukomboa bandari za Ufaransa katika bahari ya Mediterrania, ambayo pia ingesababisha vita na kuwaongezea presha Wajerumani. Hivyo mwarobaini wa kuikomboa Ulaya ikaonekana watumie majeshi toka Afrika.

Vikosi vya Ufaransa vilishiriki katika oparesheni ya kukomboa miji ya bandari ya Toulon na Marseille, Vikosi hivyo vilikuwa na changamoto kubwa ya mahali pa kutia meli nanga na pa kutua ndege zake kwa hiyo walifanya kila juhudi kuhakikisha wanafikia lengo hilo.

Wanajeshi wa Afrika walichangia theluthi mbili ya jeshi la Ufaransa mnamo mwaka 1944.Lakini operesheni ya Dragoon iliwafanya wanajeshi wa Ungereza na Ufaransa kutofautiana sana.

Uingereza ilipinga hatua nyingine ya uvamizi wa Ufaransa na badala yake ilitaka ijikite zaidi katika operesheni ya pamoja nchini Italia. Lakini tamaa ya Ufaransa kutaka nafasi zaidi ilishinda siku na kuendelea mbele na azma yake kwa kuchukua vikosi toka Afrika.

Kwa mujibu wa nyaraka za jeshi la Marekani, operesheni hiyo ilijumuisha zaidi ya wanajeshi 500,000 na karibu 230,000 kati yao walikuwa raia wa Ufaransa.

Mashambulizi yalifanywa kwa urahisi zaidi ya vita vya kwanza kwa sababu Ujerumani ilikuwa imelemazwa kutokana na shambulio la awali.

Huku operesheni ya ''Overlord'' ikichukua miezi miwili na wiki tatu kukamilika, ile ya Dragoon iliendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Ilisadikiwa kuwa ilikuwa ni operesheni iliyopata ufanisi mkubwa kwa sababu vikosi vya Ufaransa vilikomboa bandari zake, na washirika waliweza kupeleka vyakula na wanajeshi zaidi kupigana dhidi ya ukombozi na wavamizi wa Ulaya.

Winston Churchill aliipinga Operation Dragoon, akiamini kuwa vikosi hivyo vingepelekwa kupigana na Italia,hatua hiyo ilisaidia kusimamisha uvamizi wa Ujerumani nchini Ufaransa.

Inaelezwa kwamba, nguvu kazi iliyotumika katika uvamizi wa pili ilikuwa na athari ya moja kwa moja na ndiyo iliyosababisha vita baridi kati ya Marekani na Urusi.

Wanasema vikosi hivyo vingetumiwa kuzuia Muungano wa Soviet kujiimarisha Mashariki mwa Ulaya. Mawasiliano kati ya viongozi wa Uingereza na Marekani yalionyesha, Waziri Mkuu Winston Churchill na kamanda mkuu wa jeshi la Muungano, Dwight Eisenhower, walitofautiana kuhusu operesheni hiyo ya Dragoon

Wanajeshi wa Senegal waliwahi kutunukiwa nishani ya ushindi nchini Ufaransa wakati wa mwisho wa vita vikuu vya pili vya Dunia.

Inakadiriwa kuwa wanajeshi milioni moja wa Afrika walishirikana na washirika wao katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Hata hivyo George Marshall, mkuu wa utumishi wa umma wa marais wawili wa Marekani wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia (Franklin D. Roosevelt na Harry Truman) aliwahi kunukuliwa akisema ilikuwa ni moja ya operesheni iliyopata ufanisi mkubwa.

Lakini jukumu lililotekelezwa na majeshi ya kiafrika nchini Ufaransa wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia limesahaulika mpaka sasa na wengi wa wakaazi wa Bara la Afrika hawafahamu kama palitokea zoezi kama hilo kipindi hicho.

Wanajeshi wa Afrika waliondolewa nchini humo Ufaransa na Serikali ya mpito kufikia mwishoni mwa mwaka 1944.

Ufaransa iliamua jeshi lake liwe na wazungu pekee. Kwa hivyo lilichukua sare za kijeshi kutoka kwa wanajeshi weusi na kukabiliana na wale waliopinga hatua hiyo ya kuwafukuza askari weusi walioshiriki operesheni Dragoon.

Jukumu lililofanywa na mashujaa wa Afrika katika jeshi la Ufarasa wakati wa vita vikuu vya pili vya Dunia limesahaulika kama tulivyosema hapo awali.

Mamlaka nchini Ufaransa ziliongezea utata juu ya suala hilo kuanzia mwaka 1959 na kuendelea mbele, baada ya mataifa yaliyokuwa makoloni yake kupata uhuru, malipo ya uzeeni ya wanajeshi hao hayakuongezwa hadi mwaka 2010.

Lakini mwaka 2017, Rais wa Ufaransa Francois Hollande alikiri kuwa taifa hilo lina wajibu wa kufidia damu ya mashujaa wa Afrika.

Mwandishi wa habari wa Ufaransa Audrey Pulvar, ambaye alishiriki kampeni ya utambulisho wa jukumu la wanajeshi wa Afrika katika vita vya ukombozi anakumbuka na kupata picha ya mji wa Paris jinsi ulivyokombolewa kutoka katika vikosi vya wanazi wa Adolf Hitler.

Wakati umewadia kwa Ufaransa kuwajumuisha wanajeshi hawa katika kumbukumbu ya pamoja ya historia yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news