NA DIRAMAKINI
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kupitia shamba la miti ya kupanda na asili la Sao Hill mkoani Iringa lililopo Wilaya ya Mufindi wamesema, majanga ya moto yamepungua kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakitoa mara kwa mara juu ya madhara yanayotokana na moto.
Baadhi ya vijana waliojitokeza wakiwa kwenye usaili uliofanywa katika Kijiji cha Kitasengwa Kata ya Makungu.
Akizungumza wakati wa usaili wa vijana wa kupambana na moto, Mhifadhi Mkuu Msaidizi Tarafa ya Nne Mgololo,Lukiko Maiila amesema kuwa, wamekuwa wanaajiri mara kwa mara wafanyakazi kwa ajili ya kupambana na moto katika tarafa hiyo.
Maiila amesema kuwa, wamekuwa wanasaidia kuzima na kupambana na moto kipindi ambacho kunakuwa kumetokea kwa majanga hayo.
Maiila amesema kuwa, wamekuwa wanatoa elimu mara kwa mara juu ya madhara ya moto kwa wananchi wote wanaolizunguka shamba la miti la Sao Hill.
Amesema kuwa, wamefanya usaili wa vijana 137 kutoka Vijiji 12 na wanaotakiwa kuajiriwa ni vijana 49 katika Kijiji cha Kitasengwa Kata ya Makungu.
Maiila amesema kuwa, wamefanya usaili wa ukakamavu kwa sababu maeneo ambayo wanaenda kufanyia kazi yana miinuko mingi, hivyo walipokuwa na utimamu wa mwili hataifanya kazi inavyotakiwa.
Amesema kuwa, Yarafa ya nne ya shamba la Sao Hill wanatarajia kuajiri wafanyakazi 2000 ambao watakuwa wanafanya kazi mbalimbali katika tarafa hiyo kwa lengo la kulinda na kuitunza miti ambayo ipo katika shamba la Sao Hill.
Maiila alimazia kwa kusema kuwa, hawatarajii kupata majanga ya moto katika kipindi hiki cha kiangazi ambacho mara nyingi majanga hayo ndio hujitokeza.
Kwa upande wake baadhi ya wananchi wanaolizunguka shamba hilo wamesema kuwa, limesaidia kutoa elimu ya madhara ya moto na kupunguza majanga ya moto kutokea mara kwa mara.
Walisema kuwa elimu ambayo imekuwa ikitolewa mara kwa mara imesaidia wananchi wengi kuwa na uelewa mpana wa namna gani ya kuzuia kusitokee janga la moto.