NA CHARLES REGASIAN
Dahmer alizaliwa Mei 21,1960, eneo la West Allis, Wisconsin nchini Marekani na alifariki dunia Novemba 28, 1994, akiwa na umri wa miaka 34. Kifo chake kilitokana na kipigo kutoka kwa rafiki yake wa karibu aliyetajwa kwa jina la Christopher Scarver.
Sygma via Getty Images / Getty Images.
Kwa mujibu wa ripoti za polisi Dahmer aliwaua watu 17 kati ya mwaka 1978 hadi 1991 na kati ya hao aliwadhalilisha kimapenzi kabla ya kuondoa uhai wao, Dahmer kama walivyo wauaji wengine ambao hulenga kundi fulani,huyu naye aliwalenga na kuwaangamiza Wamarekani weusi na Wahindi. Kwa hakika alikuwa mtu katili sana, kwani kabla ya kuwaua aliwabaka au kuwalawiti mateka wake.
Lakini mbali na hilo, Dahmer hakuishia hapo,baadhi ya watu aliowaua alikula nyama zao kwa namna ya ajabu kabisa, baba wa Dahmer alikuwa mkemia aliyebobea, Alipofikisha umri wa miaka kumi kijana huyo hakuwa mzungumzaji mzuri na mara nyingi alipenda kujitenga na watoto wenzake,hilo likaanza kuwashangaza wazazi wake,hakuwa mtoto wa kupenda michezo wala kujichanganya katika burudani nyinginezo za watoto.
Alipofikisha umri wa miaka 15, Dahmer akaanza kuonesha tabia nyingine ya ajabu ya kuzunguka nyuma ya nyumba za majirani kusaka wanyama waliokufa na kuwaleta nyumbani. Kuna wakati fulani alionekana akila mbwa. Hali iliendelea kuwa hivyo na wakati huo huo alianza kutumia pombe, na hata siku alipokuwa akimaliza elimu yake ya sekondari wengi walimshuhudia akiwa chakari kwenye mahafali.
Mwaka 1977, baba yake alitalikiana na mkewe,Wakati huo Dahmer alikuwa masomoni katika chuo kikuu cha Ohio, lakini alishindwa kuendelea na masomo kwa vile muda mwingi alitoroka vipindi darasani. Alitumia muda mwingi kunywa pombe,baada ya kuona maendeleo ya mwanae ni mabovu baba yake alimwamuru ajiunge na jeshi.
Katika siku za mwanzo alifanya vema jeshini, lakini baada ya miaka miwili akafukuzwa kutokana na kukithiri katika unywaji pombe, baada ya kutimuliwa jeshini mwaka 1981jeshi lilimpa tiketi ya ndege na kumtaka aende sehemu yoyote ndani ya Marekani. Dahmer akawaambia Polisi kwamba asingeweza kwenda nyumbani kumkabili baba yake kwani alihisi "moto ungewaka baina yao".
Badala yake akaelekea pwani ya Miami huko Florida kwa kile alichosema kuwa, alikuwa amechoshwa kuishi maeneo ya baridi.
Hifadhi pekee huko ikawa ni hospitali, lakini baada ya muda mfupi alifukuzwa hospitalini hapo kutokana na kuendekeza ulevi, kwa hali hiyo Dahmer kama mwana mpotevu akaamua kurejea nyumbani ambako pia aliendelea kuwa mlevi wa kupindukia.
Hali hiyo ilisababisha atiwe nguvuni, kwani wakati akiwa ameshautwika alikuwa na tabia mbaya kwa raia wengine, mwaka 1982 Dahmer akaenda kuishi na bibi yake eneo la West Allis, alidumu huko kwa miaka sita mfululizo, ni kipindi hicho, tabia yake iliendelea kubadilika kwa namna ya kutisha, bibi yake aligundua nguo ya kike chumbani kwa Dahmer.
Siku nyingine akaweka bunduki uvunguni mwa kitanda, mbali na matukio hayo kukaanza kusikika harufu mbaya ndani ya nyumba yao, alipoulizwa akasema kuwa alikuwa ameleta nguchiro mfu na kwamba alimmwagia tindikali.
Kutokana na matukio ya wizi na masuala yasiyoeleweka alikamatwa mara mbili na katika tukio jingine baya alithubutu kujichua sehemu za siri mbele ya wavulana wawili.
Mwaka 1988, bibi alimwamuru aondoke nyumbani kwake kwa sababu ya tabia ya ulevi na kuchelewa kurudi nyumbani, bibi alikuwa amechoshwa na tabia za ajabu zilizoonyeshwa na mjukuu wake, Dahmer akapata makazi mapya eneo la Milwaukee, Septemba 26,1988, alikamatwa kwa tuhuma za kutumia dawa za kulevya na kosa la kumlawiti mvulana wa miaka 13 alipata adhabu ya miaka mitano, lakini miezi miwili baadae akapata msamaha wa wafungwa.
Baada ya kuwa huru,akaanza mauaji na hatimaye kunaswa mwaka 1991, kwa rekodi zilizopo,Jeffrey Dahmer, alianza kuua mwaka 1978, wakati huo akiwa bado anaishi katika familia ya baba yake, mtu huyo wa kwanza kumuua anatajwa kuwa ni Steven Hicks, ambaye alimlazimisha kunywa bia nyuma ya nyumba ya baba yake na kisha kumlazimisha kumlawiti.
Baada ya Hicks kugoma kulawitiwa,Dahmer akamtwanga na kitu kigumu kichwani na kuuzika mwili wake nyuma ya nyumba hiyo ya baba yake.
Mtu wa pili kunaswa na Dahmer ni Steven Tuomi,baada ya kufanikiwa kumuua Tuomi,Dahmer aliendelea na mauaji na mara nyingi watu aliowapata kirahisi ni mashoga.
Alikuwa akiingia kwenye baa za mashoga na kuwapa pombe na kisha kuondoka nao kwa maelewano kwamba anaenda kuwalawiti kwa malipo, baada ya kuwalawiti kilichofuata ni kuwaua na kutokomea, katika hali ya kushangaza alihifadhi fuvu la shoga mmoja,Anthony Sears aliyemuua mwaka 1969. Fuvu hilo alikutwa nalo alipotiwa mbaroni.
ZINGATIA
Mzazi ana
kila sababu ya kuwajibika katika malezi ya mtoto au watoto. Wapo wazazi
ambao wanadiriki kusema kuwa huyu mtoto amenishinda, mbele ya huyo mtoto
unafikiri hapo unamtengenezea mtoto mazingira gani na wewe pia
unajitengenezea mazingira gani? Zingatia hatua hizi;
1) Mpe malezi bora
Mlee
katika njia impasayo naye hatoiacha mpaka atakapokuwa mzee. Mlee kwa
upendo naye atakulipa kwa upendo, hakika mtoto wako ukimlea vizuri
anafuata maadili mazuri na maadili mazuri anayapata kutoka kwa mzazi,
waweke watoto wako katika hali ya usafi hata mgeni akitokea atavutiwa na
mtoto wako na hata kumpakata kuliko kumuacha mtoto mchafu muda wote
hana uangalizi anacheza katika mazingira hatarishi.
Wazazi siyo
vema kuwatukana watoto chunga sana ulimi wako, unapomtukana mtoto anaiga
matusi na tabia mbaya kutoka kwako mzazi, ataona ni kitu cha kawaida
hata mama au baba ana
2) Mfundishe mtoto jinsi ya kuvua samaki na siyo kumpa samaki
Anza
kumjengea tabia nzuri mtoto angali akiwa mdogo mpe njia za kufanikiwa,
wewe kama mzazi umepitia mengi hivyo basi kupitia makosa yako umejifunza
mengi sana kwa hiyo mfundishe mtoto apite njia nzuri ili asije kurudia
makosa kama yako,mfundishe mabadiliko ya yanayoendelea duniani ili
ajiandae na mabadiliko hayo.
Usimlee tena katika mfumo wetu wa
elimu ambapo unaandaliwa kuwa mwajiriwa, mlee katika mawazo ya
kujitegemea, kujiajiri, jinsi ya kuona fursa katika jamii na kuzitendea
kazi, jinsi ya kutengeneza ajira na siyo kuajiriwa tu kwani kazi za
maofisini siku hizi zimekuwa changamoto hivyo basi ni vema kumwandaa
mwanao katika mabadiliko haya ambayo yapo na yataendelea kuwepo.
3) Usimnyime mtoto adhabu anapokosea
Mtoto ana haki ya kuadhibiwa pale pale tu anapofanya makosa ambayo anastahili kuadhibiwa.
Sasa
kuna wazazi wengine wanalea mtoto kama yai mtoto anageuka mfalme ndani
ya nyumba au mtawala, mzazi hana kauli mtoto anafanya chochote
anachojisikia ndani ya nyumba kama vile kuvunja vitu na kuharibu bila
hata kumpa adhabu ili akome tabia hiyo.
Mtoto anatukatana watu,
na wakati wengine wazazi nao huwa wanatukanwa na watoto wao yote haya ni
kwa sababu ya kukosa malezi bora, unamnyima adhabu ndio matokeo yake
tabia inakuwa na mtoto umleavyo ndivyo akuavyo na samaki mkunje angali
mbichi.
Kwa hiyo, mtoto kuwa na kutokuwa na heshima chanzo ni mzazi umeridhika na hali hiyo ambayo mtoto wako anayo bila kuchukua hatua.
4) Mfundishe mtoto kukosa
Maisha
ya binadamu ni mafupi kwa hiyo huwezi kukaa na mwanao siku zote
inakupasa kumfundisha mtoto kukosa pia wakati mwingine ni vizuri sana
mfano mtoto anataka kitu fulani analia ameshasoma saikolojia yako mzazi,
wewe ukiona tu mtoto analia unamtimizia hata kama kitu siyo cha maana
anampa tu hata kama una hela muda mwingine mwambie sina ili ajifunze
kukosa mpe hata siku nyingine ,waingereza wanasema hivi’’ teach your
child to learn or to face disappointment’’ maana yake tuwafundishe
watoto kukosa au kukutana na changamoto ili wajifunze.
5.
Mwisho, wape watoto chakula bora ambavyo vitawapa afya bora ya mwili na
kinga dhidi ya magonjwa na hapa nazungumzia vyakula vya asili na siyo
vya viwandani kama vile matunda, mboga za majani na siyo soda, pipi
biskuti nk.
Mpe
mtoto ratiba ya kusoma vitabu au mambo yake ya darasani na siyo
kuangalia tv kwa muda mrefu. Makala hii imeandikwa na Charles Regasian
kwa nyongeza ya Deogratius Kessy ambaye ni mwandishi, mhamasishaji na
mjasiriamali.